Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Gerson Lwenge amesema mchakato wa kuanzishwa kwa Mamlaka ya maji Rombo bado unaendelea na watu wa Idara ya Sheria wanalifanyia kazi,japokuwa kwa kawaida mchakato huwa unachukua muda mrefu lakini wadau wote walishirikishwa kuanzia ngazi ya Halmashauri na kuunga mkono kuanzishwa kwa Mamlaka ya Maji ya serikali
Aliongeza kuwa, mbali na Kampuni ya Kiliwater ambayo inaendesha na kusimamia miradi ya maji Rombo kulalamikiwa na wananchi,suala la uanzishwaji wa Mamlaka ya maji ni muhimu na hakuna anayeweza kuzuia kwasababu serikali inapotoa fedha kwa ajili ya miradi ya maji ni lazima fedha hizo zisimamiwe na Mamlaka ya serikali na sio Kampuni binafsi.
Mhe.Mhandisi Lwenge amefanya ziara Wilayani Rombo na kukagua vyanzo vya maji na miradi ya maji inayoendelea na kutolea msisitizo katika suala zima la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji,ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu uvunaji wa maji ya mvua, hii ni kutokana na vyanzo vilivyopo kuonekana kutokidhi mahitaji hasa katika maeneo ya ukanda wa chini na kuahidi katika miradi itakayobuniwa baadae upo uwezekano wa maji kutoka ziwa Chala kutumika kwa wananchi wa ukanda huo
Malengo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni wananchi kupata huduma ya maji kwa asilimia 85 katika umbali wa mita 400 ifikapo 2020, ambapo Wilaya ya Rombo mpaka sasa ni asilimia 57 ya wananchi wanaopata huduma hiyo,ikiwa ni wastani mzuri ukilinganisha na baadhi ya wilaya.
Katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili na milioni mia tisa (2,900,000,000) ili kukamilisha miradi inayoendelea katika Wilaya ya Rombo
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved