Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mheshimiwa Raymond Stephen Mwangwala leo tarehe 18/12/2023 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa vipengele vya Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rombo, Katibu tawala Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Katibu wa CCM (w) Rombo, Katibu Mwenezi wa CCM (w) Rombo,Wakuu wa Idara Mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Halmashauri Kuu Wilaya ya Rombo katika uwasilishaji wa taarifa hiyo.
Mkuu wa wilaya amepitia vipengele hivyo ambavyo ni Hali ya kiuchumi katika wilaya, Kupambana na umaskini na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF, Uchumi wa rasilimali maji, Vyama vya ushirika na changamoto zake, Kilimo, Ufugaji, Uvuvi , Viwanda, Biashara, Mawasiliano, Madini, Utalii, Maliasili, Ardhi, Ukimwi, Ulinzi na Usalama, Mapambano dhidi ya Rushwa, Utamaduni Sanaa na michezo pamoja na Usafirishaji na Usafiri.
Pia Mkuu wa Wilaya amewasilisha taarifa za Utekelezaji wa Miradi katika sekta mbalimbali kama vile ROMBOWSSA ,TARURA,TANESCO,Elimu Msingi na Sekondari,Afya na Utawala ambapo miradi mingi ya kimaendeleo katika wilaya ya Rombo Imekamilika na mingine michache ikiwa katika hatua za Mwisho za Utekelezaji.
Aidha kwa Changamoto mbalimbali ambazo zimeibuliwa na Wajumbe katika kikao hicho hasa katika miundombinu ya barabara na Umeme, Vyama vya Ushirika na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa pamoja zimeahidiwa kufanyiwa kazi kwa wakati.
Pamoja na hayo,Mkuu wa Wilaya amepongeza kazi kubwa iliyofanywa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali huku akimpongeza Mkuu wa wilaya aliyepita kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye utekelezaji huo wa miradi ya Kimaendeleo ya katika wilaya yetu.
Pia, Mkuu wa wilaya ameomba Ushirikiano,kushauriana na kusaidiana ili kufikia katika malengo tuliyojiwekea katika wilaya yetu ya Rombo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved