Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imefanya kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza leo Novemba 07, 2023, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo baraza limepokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza(julai - septemba).
Kikao kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali ikiwa ni kikao cha wazi.
Akipokea taarifa za utekelezaji wa kazi kutoka kamati mbalimbali za Halmashauri. Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Gilbert Tarimo amewashukuru waheshimiwa madiwani na wataalamu pamoja na taasisi mbalimbali kwa kufanikiwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi.
“Kwanza niwashukuru Waheshimiwa madiwani kwa kuweza kufanya kikao hiki cha baraza salama na kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hata hivyo Mwenyekiti amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa miradi ya maendeleo,pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Kanali Hamis Maiga na Mbunge ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda kwa kuendelea kuisemea vema Wilaya ya Rombo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved