Divisheni ya Afya, Usatawi wa Jamii na Lishe imekaa kakao cha robo mwaka ya tatu (jan -mach 2023) na kamati ya Lishe ya Halamashauri ya Wilaya ya Rombo leo tarehe 25 Mei2023 katika ukumbi wa vikao Huruma Hospitali.
Mwl. Charles Mganga aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho akimwakilisha Mkurugenzi, aliwaongoza wajumbe kutoka divisheni mbalimbali waliohudhuria kikao hicho kilichokuwa na malengo ya kupokea taarifa ya robo mwaka kutoka seksheni zifuatazo;-
Seksheni ya Lishe,
Sekheni ya Kilimo,
Sekesheni ya Mifugo na Uvuvi,
Divisheni ya Elimu ya Awali Msingi na Sekondari
Divisheni ya Maendeleo ya Jamii.
Afisa lishe wa Halmashauri ya Rombo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa viashiria vya mkatatba wa lishe katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi ambapo katika taarifa hiyo yafuatayo yalikuwa ni baadhi ya mafanikio;-
Ukaguzi wa maeneo mbalimbali yanayoshughulika na utengenezaji, uandaaji uhifadhi, na usambazaji kama vile mabucha, vichinjio, maduka ya vyakula. Lakin pia shughuli hii ilifanikiwa kufanyika kwa kushirikiana na maafisa wa afya mifugo na kilimo.
Utoaji wa matibabu kwa watoto wenye umri chini ya miaka motano (5), elimu ya ulishaji wa watoto wachanga na wadogo kwa kina mama na nwalezi katika vituo vya huduma za afya huku vituo takribani 38 vya kutolea huduma vikifikiwa katika utoaji huo wa elimu.
Ukutoa vidonge vya madini chuma na Asidi ya Filiki kwa kina mama wajawazito , utoaji wa chakula kwa wanafinzi shule za msing na sekondari zaidi sana upimaji wa uwepo wa madini joto katika chumvi.
Pamoja na mafanikio hayo bado kulikuwepo changamoto zilizoikumba seksheni ya lishe katika utekelezaji kama ifuatavyo;-
Hamasa ndogo ya wadau wanaojishughulisha na huduma za lishe katika Halmashauri
Upungufu wa vifaa vya upimaji madini joto .
Hata hivyo divisheni ya elimu nayo iliwasilisha taarifa ya utekelezaji ikiwa ni moja kati ya divisheni mtambuka katika utekelezaji wa mkataba wa lishe katika Halmashari.
Katika taarifa yao iliyowasilishwa katika kamati walionyesha mafanikio na changamoto zao kama ifuatavyo
Wametembelea shule 7 zinazofuga ngombe na kuzidi kuhamasisha ulimaji wa mboga mboga kwajili ya kuboresha lishe shuleni.
Upandaji wa miti ya matunda mbalimbali na kila shule awepo walau mwalimu mmoja wa afya na viranja wa afya katika shule ili kuzidi kutilia mkazo katika swala zima la lishe shuleni.
Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kutengewa bajeti yao yenye kiapaumbele cha kuhakikisha wanapata lishe Bora
Pamoja na mafanikio waliyyapata katika utekelezaji wa mkataba wa lishe Divisheni ya Elimu, pia ilikumbana na changamoto kama ifuatavyo;-
Uhaba wa maji hasa kipindi cha kiangazi ambacho husababisha ukame ambao hurudisha nyuma jitihada.
Uhaba wa maeneo katika baadhi ya shule kupelekea hata shule hukosa ata eneo la kupanda mboga mboga na ukosefu wa majani ya kulisha mifugo kama ngombe.
Baadhi ya wazazi kutokuwa tayari kutoa michango ya upatikanaji wa lishe kwa watoto wao shuleni.
Aidha katika kikao hicho wajumbe walikubaliana katika kuongeza jitihada zaidi katika kiboresha utekelezaji ili jamii nzima iweze kupata elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa lishe katika kulinda afya bora
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved