Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Rombo leo Aprili 24, 2024 imefanya Kikao cha kawaida cha Kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za Afya na lishe kwa kipindi cha Robo ya Tatu kuanzia Januari hadi Machi 2024.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkuu wa Dividheni ya maendeleo ya jamii Bi. Severina Kilala amesema kuwa Halmashauri ya Rombo inatekeleza maagizo ya upatikanaji wa lishe kwa vitendo kwani Serikali ya Tanzania imedhamiria kuendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe bora nchini ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara kupitia maendeleo ya viwanda, hivyo elimu ya Lishe itasaidia uwepo wa watu (nguvu kazi) wenye afya njema ili kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii na Kuchochea maendeleo ya nchi.
Katika kikao hicho Divisheni mbalimbali ziliwasiliisha taarifa za utekelezaji wa kazi za Afya na lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ambapo baada ya taarifa hizo Kamati iliweza kujadili na kutoa maelekezo kwa Divisheni ya kilimo, Mifugo na uvuvi kuhakikisha wanasimamia zoezi la uchinjaji na ukaguzi wa nyama kwa ukaribu zaidi ili kuepukana na magonjwa mbalimbali mfano ugonjwa wa kimeta.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Bi. Philiberta Rogath amesema “Kwa upande wa Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii tumeendelea kutekeleza afua za Lishe na tukifanikiwa kutoa elimu kwa Wananchi wa Kata na vijiji kupitia vikao mbalimbali kuhusu masuala ya lishe bora.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe walikubaliana katika kuongeza jitihada zaidi kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe ili kuboresha Afya na kulinda Afya zao.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved