• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA MATOKEO SEKONDARI 2022-2023

Posted on: March 22nd, 2023

Idara ya elimu, wadau wa elimu pamoja na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Rombo, wamefanikiwa kufanya kikao cha tathmini ya mwenendo wa matokeo ya kidato cha pili na kidato nne. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya saint joseph iliyopo mkuu, Rombo kililenga kufikia ufaulu wa asilimia 100 kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari kwakuwa ndipo maarifa ya msingi katika uhai na ufanisi wa maisha ya mwanadamu yalipo.

Moja ya agenda katika kikao hiko kilichohudhuriwa na wadau wa elimu mbalimbali ikiwemo waalimu, waalimu wakuu, wakuu wabodi ya shule, maafisa elimu kata na waheshimiwa madiwani, ilikuwa ni kupata taarifa ya elimu na umuhimu wa wadau wa elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata kile wanachostahili kupata shuleni.

Hata hivyo kikao hiko kilifanikiwa kuweka makubaliano ya kimkakati ya kuongeza ufaulu kwa mwaka 2023 endapo yatafanyiwa utekelezaji unaoendana na kauli mbiu isemayo “MBINU SHIRIKISHI UWAJIBIKAJI UTAWEZESHA YALIYOSHINDIKANA YAWEZEKANE”.Yafuatayo ni makubaliaono ya kimakakati yaliyopitishwa na wadau wa elimu  ambayo ni pamoja na

  • kuuongeza muda wa wanafuzi kujisomea
  • kuhimiza matumizi ya lugha ya kiingereza katika kuongea na kuandika shuleni
  • kutumia njia shirikishi zenye kujenga umahiri katika ufundishaji na ujifunzaji
  • kuhakikisha mada azote zinafundishwa vizuri, kwa ukamilifu na kwa wakati
  • kufanya tathimini kubaini maeneo yenye changamoto katikaufundishaji
  • kutumia vijitabu vya cira kufanya mapitio ili kubaini dosari zilizojitokeza katika majibu ya watahiniwa
  • kuhimiza ushindani na hamasa baina ya waalimu na wanafunzi katika kujifunza na kufundisha 
  • kuhimiza uandishi sahihi wa insha kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa
  • kuhimiza michezo na clubs mbalimbali shuleni

Aidha, afisa taaluma sekondari wailaya ambaye  ndiye aliyekuwa  mwenyekiti wa kikao hicho , aliendesha majadiliano na maazimio na wadau hao wa elimu na kusema kuwa, wilaya imejipanga kutoa motisha chanya ya Tsh 5,000/= kwa kila “A” halali, na hadi sasa Tsh 5,000,0000/= zimeshaanza kukusaanywa kwaajili ya zawadi kwa wadau wote wa elimu watakao faulisha kwa ufaulu wa asilimia 100. Lengo la utoaji wa zawadi likiwa ni kuongeza na kuchochea ufaulu kwani tathimini ya mwenendo na hali ya matokeo kiujumla hairidhishi hivyoo amewaasa wadau wote wa elimu kuchukua kwa uzito utekelezaji wa majukumu yao kama wadau wa elimu.

Katika kikao hicho mlw. Charles Daudi Mganga (Kaimu Mkurugenzi) alifanikiwa kutoa nasaa zake  na kuwaasa sana waalimu kujitoa kikamilifu katka kutekeleza majukumu yao kwani  waalimu  ndio wenye mchango mkubwa kuahakikisha ufaulu wa asilimia 100 kama yalivyo malenge.

Hata hivyo naye aliyekuwa mgeni rasmi ambae ni Katibu wa mbunge aliongeza kwa kuwatia moyo wadau wa elimu na kuahidi kuchukuwa changamoto zilizotajwa na wadau wa elimu na  kuwahakikishia atazipeleka mahala husika zipatiwe mwarobaini.

 Hali kadhalika Katika kikao hicho, ,halmashauri ya wilaya ya Rombo kupitia idira ya elimu,  ilifanikiwa kutoa vyeti na zawadi mbalimbali, ikiwemo mitungi ya gesi, sukari na mchele kwa shule zilizofanyanya vizuri, pia kwa shule zilizoonyesha jitihada na mjongeo chanya katika matokeo ya kidato cha pili na  cha nne ya mwaka 2022.

Kwa taarifa zaidi kuhusu tathimini hiyo unaweza ukaipata hapa

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved