Mhe Diwani mteule kata ya Kelamfua Mokala Gilbert Tarimo aliepita bila kupingwa kwa kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika septemba mwaka huu Leo amekula kiapo cha kuwatumikia wananchi wa Rombo mbele ya Mheshimiwa Hakimu pamoja na Baraza la Madiwani.
Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CHADEMA Frank Joseph Lubega kujiuzulu wadhifa huo na kujiunda na CCM akiunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Pamoja naye waheshimiwa madiwani wawili wa viti maalumu kutoka CHADEMA walijiuzulu na kujivua uanachama na kujiunga na CCM.
Akizungumza katika Baraza hilo Mhe.Tarimo ameshukuru kwa mapokezi mazuri aliyopata kutoka kwa waheshimiwa madiwani huku akiomba ushirikiano kutoka kwa watendaji wa halmashauri pamoja na madiwani ili kwa pamoja wasaidiane kuwahudumia wananchi wa Rombo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved