Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe.Raymond Mwangwala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo Ndg. Godwin J Chacha mapema leo wamekabidhi Pikipiki 3 kwa Watendaji wa Kata Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.
Kata zilizonufaika na Mgao huo ni Kata ya Manda, kata ya Kirua Keni
Pamoja na kata ya Kisale Msaranga
Mhe. Mwangwala aliwasihi Watendaji wa Kata kwenda kuzitumia pikipiki hizo kutolea na kufikisha huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na kuwa makini na vyombo hivyo vya moto sambamba na kuvitunza.
Kadhalika Mhe Mwangwala amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha Watendaji wa Kata na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved