• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Wananchi Rombo wahofiwa kula nyama zisizokaguliwa

Posted on: October 16th, 2019

Hofu iliyokuwa miongoni mwa waheshimiwa madiwani juu ya nyama zisizokaguliwa na wataalamu wa mifugo kuuzwa na kuliwa na wananchi imeondolewa baada ya Daktari wa Mifugo Dr Emil Mkemwa kuwahakikishia kuwa nyama zote zinazouzwa kwenye mabucha rasmi zimekaguliwa na ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Waheshimiwa madiwani waliibua hoja hiyo katika kikao cha kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira, ambapo  walizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na kukihakikishia kikao kuwa kuna baadhi ya wafugaji ambapo hujifanya wao ni wataalamu wa mifugo na kuchinja mifugo na kuuzia wananchi bila kukaguliwa na wataalamu kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wananchi wa Rombo.

Akijibu hoja hiyo Dr Mkemwa  amesema kuwa japokuwa kuna changamoto ya Idara ya Mifugo kuwa na wataalamu wa Mifugo 15 tu, lakini kwa uchache wao hujipanga na kuhakikisha nyama zote zinazochinjwa na kuuzwa kwenye mabucha rasmi zinakaguliwa na ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Hata hivyo ameomba ushirikiano baina ya wataalamu wa mifugo  na waheshimiwa madiwani  kupeana taarifa iwapo kuna wafugaji na wafanyabiashara wasio waaminifu katika maeneo yao,  ambao wanawakwepa wataalamu wa mifugo na kuchinja mifugo inayoumwa bila kujua imeumwa nini au kuuza nyama ya mizoga ili hatua stahiki zichukuliwe.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Athuman  Kimaryo  diwani wa kata ya  Mrao Keryo amesema kuwa  kiuhalisia bado wananchi wengi wanakula nyama ambayo haijakaguliwa kwasababu  kuna wananchi wanachinja saa 9 usiku na ikifika saa 11 alfajiri nyama imeshauzwa imemalizika na pindi mtaalamu wa mifugo akifika hakuti kitu, hivyo tatizo kubwa analoliona hapo ni uhaba wa wataalamu  na baadhi yao si waaminifu.

Naye diwani wa Kata ya Tarakea  Motamburu Mhe. Beda  Moshi amesema kuwa sio rahisi kwa wataalamu kuwapitia wananchi wote hata kama wakiwepo wanne katika kata moja kwasababu kila mtu anachinjia nyumbani tena wanyama wanaochinjwa ni tofauti tofauti hivyo bado usalama wa nyama zinazoliwa na wananchi ni mdogo  ila anaona ingekuwa vyema kama kungekuwa na centre  maalumu ya kuchinjia ingekuwa rahisi zaidi kufanyiwa ukaguzi.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved