Severine lasway diwani wa Shimbi Kwandele achaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20,
Madiwani walioshiriki uchaguzi walikuwa ni 33 kati ya 37 waliopaswa kuwepo lakini madiwani wanne hawakuhudhuria kikao kutokana na dharura mbalimbali. Katika uchaguzi huo Mhe. Severine wa CHADEMA alipata kura 31 na mpinzani wake Abdala Mbago wa CCM alipata kura 2 na hakukuwa na kura zilizoharibika.
Kwa matokeo hayo Mhe. Severine Michael Lasway kwa tiketi ya CHADEMA alitangazwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20.
Awali uchaguzi huo ulishindwa kufanyika kutokana na wagombea kutofikisha asilimia hamsini ya kura zote kitu kilichosababisha kuahirishwa kwa zoezi hilo kwa muda ili kuchagua wagombea upya .
Baraza la madiwani wilaya ya Rombo linaloundwa na madiwani 38 wakiwemo wa kuchaguliwa na viti maalum, lina jumla ya madiwani 35 wa CHADEMA , 2 wa CCM na mmoja amejiuzulu na kurudi CCM.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved