Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera bunge na uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amefanya ziara wilayani Rombo leo tarehe 19 julai na kupokelewa na Mkuu wa wilaya Mhe. Kanal Hamis Maiga Pamoja na viongozi na watumishi mbalimbali kutoka halmashauri.
Naibu Waziri Ummy katika ziara hiyo aliongozana na katibu wa (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro na kufanikiwa kutana na wanachama wa (UWT) wa wilaya ya Rombo. Mhe. Ummy alisomewa taarifa ya mwenendo wa chama cha UWT wilaya ya Rombo ikiwemo malengo, mafanikiao pamoja na changamoto zinazowakunba wanachama hao.
Baada ya kusikiliza na kupokea taarifa hiyo Mhe.Ummy aliweza kutoa hamasa kwa wanchama hao kwa kuwachangia nondo pamoja na mifuko saruji kwaajili ya ujenzi wa nyumba za makatibu wa (UWT) wilaya Rombo. Pia mhe.Ummy aliweza kutoa majiko ya gesi 75 kwa wanachama hao ikiwa ni juhudi za kuwatuwa wakina mama kuni kichwani.
Vilevile viongozi wa UWT wakishirikiania na mhe. Ummy walimkabidhi mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe. Maiga cheti cha heshima kwa kazi kubwa na mchango wake katika kuhakikisha wanachama hao wanapata ushirikiano wakutosha katika kutimiza malengo yao.
Mheshimiwa Naibu Waziri pia alifanikiwa kutembelea shule ya msingi Mreai iliyopo katika kata Ubetu kahe yenye kufundisha Watoto wenye uhitaji maalumu. Mkuu wa shule alisoma taaarifa fupi kushusu Shule, mafanikio changamoto Pamoja na malengo.
Katika taarifa hiyo, kulionekana kuwepo kwa changamoto ya vifaa vya kufundishia, uhaba wa waalimu pamoja na Watoto hao kukosa mwendelezo baada ya kuhitimu darasa la saba. Hivyo wakaomba serikali iweze kuwatatulia changamoto hizo ili kuboresha utoaji huduma shulen hapo.
Mhe. Ummy alipokea taarifa hoyo na kusema atafikisha sehemu husika ili kuweza kuchukuliwa hatua zaidi hivyo akawasihi waalimu wa shule hiyo kuwa na Subira huku serikali ikayatafutia mwarobaini changamoto zao. Mhe ummy pia alitoa agizo kwa kutoa kwa wananchi wenye Watoto wenye ulemavu kuwapeleka Watoto shule kikatiba ni haki ya kila mtu kupata elimu. Katika kusisitiza hilo Mhe. Ummy aliweza kujitolea mfano kuwa endepo wazazi wake wasingempeleka shule kisa ulemavu wake basi leo hii asingeweza kuwa naibu Waziri.
Mwisho kabisa Naibu waziri aliweza kukabidhi baskeli mbili maalum kwa watu wenye walemavu katika kituo cha watu wenye mashima iliyopo kata ya ubetu kahe baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo katika kata hiyo ya Ubetu Kahe.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved