Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh.Raymond Mwangwala akikabidhi hundi ya mfano kwa vikundi vya walemavu,wanawake na vijana shilingi milioni mia sita,arobaini na moja,laki sita ishirini na mbili elfu,mianne thelethini na mbili (641,622,432).
Fedha hiyo ni mkopo unaotelwa na Halmashauri kuwawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kuachana na mikopo umiza.
kiasi hicho cha fedha ni awamu ya pili iliyotolewa na Halmashauri kwa vikundi 52,ikiwa na jumla ya vikundi vya wanawake 24, Vijana 13 na walemavu 15.
Ikumbukwe awamu ya kwanza ya mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri Wilaya ya Rombo ilitolewa kiasi Milioni mianne,kumi na saba na laki nne kwa vikundi vya wanawake 7,vijana 5,walemavu 2 na kuwa na jumla ya shilingi Bilioni moja,milioni hamsini na tisa,ishirini na mbili elfu mianne thelethini na mbili(1059,022,432).
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved