Halmashauri ya wilaya ya Rombo imetoa mafunzo kwa Vikundi vya wanawake wajasiriamali walioomba mikopo halmashauri chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana
Katika mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Bi Sapiencia Mugarula aliwahamasisha wanawake kujiunga katika vikundi ili wapate mikopo kwasababu halmashauri inatoa mikopo kwa vikundi na si mtu mmoja mmoja, hivyo ni muhimu kwao kama kikundi wafanye kitu kitakachowaweka pamoja kama vile biashara ya pamoja.
Vilevile aliwaasa kutokuwa watumwa wa mikopo kwa kutambua na kuelewa faida na matumizi sahihi ya mkopo ikiwa ni pamoja na kuzijua fursa za kifedha, athari za matumizi mabaya ya fedha na jinsi ya kupata faida na kujiongezea kipato,kwa kutambua hayo itasaidia kuepuka kukopa mikopo isiyowaingizia faida na badala yake kuzidi kuwanyonya kiuchumi hata marejesho ya mkopo yanakuwa ya kusuasua.
'lengo la mkopaji ni kutatua shida na kupunguza ukali wa maisha hivyo basi kuchukua mkopo ni jambo zuri na la msingi lakini mkopo una marejesho yake ambayo mkopaji anatakiwa kurejesha kwa kipindi alichowekewa hivyo ni muhimu kuzingatia hilo ili kutokana na marejesho hayo yatawapa fursa na wengine kupata mkopo ambao utawasaidia kuanzisha biashara itakayowainua kiuchumi'. alimalizia
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved