Ujenzi unaoendelea wa daharia katika shule ya sekondari Motamburu utawarahisishia wanafunzi waliokuwa wanatembea umbali wa kilometa 12 hadi 27 kufika shuleni hivyo kupunguza mazingira hatarishi kwa wanafunzi ambayo yanasababisha mimba za utotoni, ajali kutokana na matumizi ya usafiri usio rasmi na utoro.
Mradi huo ambao ulikuwa umepangwa kutekelezeka kupitia ufadhili na michango ya wananchi ulikadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 194,775,684, mpaka sasa upo katika hatua nzuri baada ya Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) kufadhili mradi huo kwa kuchangia kiasi cha kiasi cha shilingi 150,000,000.
Kwa upande wa ushiriki wa wananchi katika mradi huo ni upatikanaji wa eneo ambalo lina gharama ya shilingi 10,000,000 ambapo kujengwa kwa daharia hiyo kutawanufaisha wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kutoka katika maeneo ya Nalemuru,Endonet na Kamwanga.
Mpaka sasa kazi zilizobakia katika ujenzi huo ni kuweka dari, vioo na kupaka rangi. Daharia hiyo ina vyumba 20 vya kulala wanafunzi ambapo kila chumba kinachukua wanafunzi wanne, hivyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 wa bweni.
Ujenzi huo pia umezingatia uwepo wa nyumba ya matroni na miundombinu muhimu na rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu vitu vitakavyosaidia kuwalinda watoto wa kike na kuinua maendeleo ya kitaaluma katika shule hiyo ambayo mpaka sasa ni ya wastani kutokana na wanafunzi kutohudhuria masomo ipasavyo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved