• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Uharibifu wa chakula ni uhalifu-DC Hokororo

Posted on: November 1st, 2018

Mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe. Agnes Hokororo  amepiga marufuku kwa wananchi kuruhusu mifugo kutoka nchi  jirani ya Kenya kufanya malisho mashambani  na kufanya uharibifu wa mazao ya chakula ,kwa sababu wakaazi wa Rombo wanafanya ufugaji  wa ndani  hivyo si vema kuruhusu mifugo ya watu wengine kuzurura.

Ameyasema hayo alipokuwa anasikiliza kero mbalimbali katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Kiwanda mapema leo ,ambapo  wananchi walilalamika mazao yao kuliwa yakiwa shambani na mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya ,na  wanapokuja kulisha mifugo wanakuja na silaha mbalimbali kama mapanga na sime.

Ameongeza kuwa pale inapotokea kuna makubaliano ya kibiashara ya kuuziana malisho kati ya Mkenya na Mtanzania basi ni vema aandaliwe kwa kukatiwa majani au mahindi na kupewa aondoke nayo ili kuepusha uharibifu wa mazao ya wengine mashambani kwa kuwa anapoingiza mifugo shambani hawafanyi malisho  eneo moja tu walilouziwa bali wanaharibu na mazao ya mashamba jirani.

“Uharibifu wa chakula ni uharibifu wa mali kama zilivyo mali zingine, Kaimu Kamanda wa Polisi wilaya nakuagiza, kama ambavyo tunakamata wahalifu katika maeneo mengine na hawa ni wahalifu vilevile kwasababu chakula ni hitaji muhimu katika jamii  kwa maendeleo ya kila siku”.alisema Hokororo

Pamoja na hilo ameushauri uongozi wa kijiji kuunda kamati imara ya kusimamia masuala ya mazingira ikiwa ni pamoja na  kuweka ulinzi wa kutosha kwa kila mtu kuwa mlinzi wa jirani yake ili kuwatambua wanaoruhusu malisho kwenye mashamba bila idhini ya wenye mashamba.

Wizara ilishatoa  onyo kuhusu mifugo kuzurura ovyo  pamoja na maelekezo ya kufuata sheria za NARCO ambazo zinaelekeza gharama za kuchangia mifugo inapofanya  uharibifu wa mazingira, nyasi walizokula , maji na mengineyo.

Kwa upande wa wanyama waharibifu kama Nyani,  Mhe. Hokororo amemuagiza Afisa Ardhi,maliasili na mazingira  kutafuta mbinu mbadala ya kuwafukuza bila kuwadhuru ili wasiendelee kuharibu mazao,

 Vile vile amewaelekeza wananchi pindi  wanyama wakubwa kama Tembo na wengine wanapokuja kushambulia basi ni budi kuandika barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ili wizara husika ipewe taarifa kwa ajili ya fidia inayotolewa kwa mujibu wa sheria

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved