• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Tamu na chungu ya Jani la Sale

Posted on: November 18th, 2019

Jani la sale ni maarufu miongoni mwa kabila la wachaga, ni jani linaloheshimika sana katika  kutatua migogoro na kuombea msamaha . Kwa imani za kichaga mtu yeyote aliyekosea akienda  kuomba msamaha na jani la sale basi ni budi asamehewe. Lakini pia jani hili hutumika kuwekea mipaka ya maeneo na kukaribishia wageni kama viongozi wa dini na serikali kuashiria amani .

Jani hili ambalo kwa uhalisia wake lilikua linasaidia kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa kabila la wachaga limegeuka kuwa shubiri katika jamii ya wachaga kwasababu limekuwa likizorotesha  mchakato mzima wa kutafuta haki, na linachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matendo ya ukatili pamoja na  mimba za utotoni.

Kamati ya MTAKUWWA( Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto) wilaya ya Rombo imeazimia  kuundwa kwa sheria ndogo dhidi ya matumizi ya  Jani la sale kwenye kesi za ukatili wa kijinsia, baada ya kuonekana kesi nyingi za ulawiti, ubakaji na mimba zinamalizwa kimila kwa kutumia majani hayo.

Aidha  baadhi ya wajumbe wa  kamati hiyo wamesema kuwa jani la sale limekuwa halitumiki tena kama jani la amani bali ni kama jani la kuvunia fedha,kwani katika mchakato wa kutatua kesi kimila sio jani la sale pekee linalotumika huwa linaambatana na fedha au mifugo ili mhusika kusamehewa.

Pamoja na hilo kuna baadhi ya wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA walilishutumu jeshi la polisi wilaya ya Rombo kwa kuzorotesha upatikanaji wa haki kwa kutoshirikiana na wananchi kupinga vitendo vya ukatili kwa kuwaachia huru watuhumiwa.

Katika kujibu tuhuma hizo Mkuu wa Polisi (W) Ndg Ally Kitole ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, amesema kuwa hakuna kitu kinachomshangaza kama kesi za Jinai kutatuliwa kimila hasa kwa kutumia majani ya Sale, na kuongeza kuwa haki jinai haitegemei mtu mmoja kupatikana, na wananchi  ndio wamekuwa wakichangia kukwamisha mchakato mzima wa kupata haki , kwani muathirika mwenyewe ndio anakuwa wa kwanza kutotoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe. Agness Hokororo akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya wilaya kilichofanyika Nov,15 2019 ameelezea masikitiko yake juu ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili na ukwamishaji wa haki pale ambapo wananchi wanakwamisha mchakato wa utafutaji wa haki kisheria.

 Amesema kuwa kesi nyingi za ulawiti na ubakaji katika mahakama ya wilaya zimeshindwa kuendelea kutokana na mzazi (mama) anapoitwa mahakamani kutoa ushahidi, wamekuwa wanaficha ukweli,hivyo kufifisha haki za watoto wao hasa pale wanapoamua kukubaliana na kumalizana na watuhumiwa.

Aidha Hokororo amezungumzia vitendo vya ukatili na mauaji ambavyo  vimekithiri katika wilaya ya Rombo hasa katika Tarafa ya Usseri ambapo kwa mwaka huu 2019 kuanzia Aprili hadi July  jumla ya watu wasiopungua  nane (8) waliuawa na kwa bahati mbaya jeshi la polisi lilishindwa kuhakikisha wahusika wanatiwa nguvuni  kwa sababu walikosa ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Sambamba na hilo ameongelea matukio ya wanaume kujinyonga  katika eneo la Rombo , kitu ambacho pengine kwa kiasi kikubwa kinachangiwa na  vitendo vya ukatili na unyanyasaji wanavyofanyiwa wanaume, huku akisisitiza kuwa  matendo ya ukatili na unyanyasaji wanafanyiwa makundi yote hata wababa lakini hayaripotiwi.

Hokororo ametoa rai kwa viongozi wa dini wasisite kusemea  wazi wazi vitendo vya ukatili na unyanyasaji  katika makanisa na misikiti kwa kutumia maandiko ya dini  ili jamii ibadilike, kwa sababu matendo hayo ni kinyume na mpango wa Mungu.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved