Baadhi ya Maafisa Elimu kata wakizifanyia Majaribio pikipiki walizogaiwa kwa dhumuni la kuwarahisishia kuzunguka katika kata zao ili kutimiza majukumu yao kwa urahisi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Bi. Magreth John leo tarehe 13.10.2018 Amewakabidhi Maafisa Elimu kata pikipiki ishirini na saba (27) zilizotolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa Elimu kupitia Mpango wa kukuza stadi za KKK yaani kusoma,kuandika na kuhesabu ili kuinua kiwango cha Elimu nchini.
Aidha amewaagiza maafisa Elimu kata kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo kwasababu changamoto ya usafiri imeshatatuliwa na serikali, ikiwa ni pamoja na kuelimisha wananchi kuwaandikisha watoto wao shule pamoja na kuondoa au kupunguza utoro mashuleni.
Aliongeza kuwa ni muhimu wahakikishe wanasimamia vyema rasilimali za shule bila kusahau kuwasimamia wakuu wa shule kuhakikisha wanafanya matumizi sahihi ya Fedha za serikali kwa kufuata miongozo.
Naye Kaimu Afisa Elimu Sekondari(W) Ndg Vianne Mgoma ametoa rai kwa Maafisa Elimu Kata kuwasimamia walimu vizuri hasa wale ambao wamekuwa hawafiki kazini au wanafika lakini hawafundishi ipasavyo hii inatokana na urahisi watakaokuwa nao sasa wa kufika katika maeneo wanayoyasimamia kwa wakati.
Naye Katibu wa TSC(W) Emmanuel Mwaimu amewatahadharisha Maafisa Elimu Kata akitumia kanuni na. 8 ya 2003 na kanuni na 42 ya utumishi wa umma kuwa moja ya makosa ya kinidhamu ni kutumia mali ya umma kwa matumizi binafsi, na uzembe unaosababisha hasara kwa muajiri adhabu zake ni fidia au kulipa gharama lakini pia unaweza kushtakiwa au kufukuzwa . Hivyo ni vema wakizijua kanuni hizo ili wajue mali za umma zinavyotakiwa kutumika.
Mwakilishi wa Maafisa Elimu kata(jina lake limehifadhiwa) alishukuru kwa niaba ya wenzake na kumuahidi Mkurugenzi Mtendaji kuwa watatizimiza maelekezo yote waliyopewa ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani.
Pia alichukua fursa hiyo kumshukuru kwa kuwapatia mafunzo ya udereva wa pikipiki kabla ya kuwagawia pikipiki hizo kwani ameonesha anawajali wao na usalama wao.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved