• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Serikali kuboresha usikivu wa TBC Rombo

Posted on: January 13th, 2020

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe  amefanya ziara wilayani Rombo na kukagua usikivu wa matangazo ya Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC) , ikiwa ni pamoja na kutembelea mtambo wa kurushia matangazo uliopo katika eneo la Tarakea.

Dkt .Mwakyembe amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 E imeweka wazi  jukumu la serikali kuhakikisha wananchi wanapata taarifa. Na kwa kutambua hilo wizara kwa kushirikiana na sekta ya mawasiliano iliunda timu iliyopita kukagua maeneo yote ya mipakani ambayo ndio yenye shida ya kupata usikivu na kukuta wanasikiliza redio za nchi jirani.

Baada ya kupita timu hiyo Dkt Mwakyembe amesema kuwa changamoto za usikivu zilitatuliwa katika maeneo mengi lakini bado serikali iliendelea kupata malalamiko katika maeneo ya Rombo na Loliondo na baada ya timu ya pili kupita pia iligundua bado maeneo hayo hayana usikivu.

‘Kwa  wilaya ya Rombo ni lazima kufanya uwekezaji zaidi, kwa kuweka Mtambo zaidi ya mmoja na kuuongezea nguvu Mtambo wa kurushia matangazo uliopo Moshi ili eneo lote la Rombo lipate usikivu wa TBC’, amesema Dkt. Mwakyembe.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TBC, Mhandisi  wa Ufundi Upendo Mbelle amekiri kuwepo kwa changamoto ya usikivu katika baadhi ya maeneo baada ya Shirika kufanya ukaguzi wa mitambo na kubaini changamoto ya kila mtambo.

 Ameongeza kuwa TBC imejipanga kufanya maboresho katika mitambo yao na tayari vifaa vyote vinavyotakiwa vimeshanunuliwa, kwa sasa vinafanyiwa uhakiki na ndani ya miezi mitatu kazi ya maboresho itakuwa imekamilika.

Aidha kwa upande wa wilaya ya Rombo Mhandisi Mbelle amesema kuwa maboresho yatafanyika katika mtambo wa kurushia matangazo uliopo Moshi ili usikivu ufike mpaka eneo la Holili, na vilevile wataongeza mtambo mwingine katika eneo la Mkuu ili eneo lote la Rombo lipate usikivu.

Awali akimkaribisha Dkt Mwakyembe , Mkuu wa wilaya ya Rombo Agness Hokororo amesema kuwa kero kubwa kwa wananchi wa Rombo baada ya Maji ni mawasiliano, kitu kinachoweza kupelekea watu kupashana habari zisizo sahihi.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved