DC Hokororo akizungumza na wadau wa Elimu
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agness Hokororo amesema kuwa wilaya ya Rombo imependelewa na Wizara kwa kuletewa fedha za kutekeleza miradi miwili ya elimu kwa mwaka 2019, ikiwa ni milioni 152 za kujenga ofisi za udhibiti ubora wa shule na milioni 500 za kukifanya upya chuo cha maendeleo ya wananchi Mamtukuna kilichokuwa chini ya Maendeleo ya Jamii ambacho kwa sasa kinasimamiwa na wizara.
Hayo ameyazungumza katika halfa fupi ya ufunguzi wa Ofisi ya udhibiti ubora wa shule uliofanyika mapema leo Januari 29,2020
Ameongeza kuwa serikali ipo mstari wa mbele kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuimarisha miundombinu mbalimbali katika sekta za elimu,afya ,barabara na umeme bila kujali itikadi,rangi dini wala ukabila na wananchi wa wilaya ya Rombo ni wanufaika.
Katika hatua nyingine Hokororo amewataka wadau wa elimu kutoiona ofisi ya udhibiti ubora wa shule kama washitaki ,bali wafanye kazi kwa kushirikiana kunyanyua kiwango cha elimu na ufaulu kwa wilaya kwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kusomea kwa walimu na wanafunzi.
Naye mdhibiti ubora kanda amesema kuwa suala la udhibiti ubora ni mfumo unaoangalia viwango vya elimu na kazi hii inafanyika kwa ushirikiano kuanzia ngazi ya shule ambapo mdhibiti ubora ni mkuu wa shule akishirikiana na baadhi ya walimu, wadhibiti ubora wengine ni Afisa elimu kata, Afisa Elimu(Wilaya) Afisa Elimu(Mkoa) ,wote kwa pamoja wanashirikiana kuhakikisha shule zinafanya vizuri na kuwa na ufaulu wa kutosha
Akisoma taarifa fupi ya mradi Mdhibiti ubora wa shule W amesema kuwa wilaya ya Rombo ni miongoni mwa wilaya 100 zilizopewa fedha ya kujenga ofisi za Udhibiti ubora wa shule Tanzania ambapo kwa kanda ya kaskazini yenye jumla ya halmashauri 18 Rombo ni Miongoni mwa wilaya 10 zilizofanikiwa kupata fedha za ujenzi .
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved