• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Rombo,Alvsbyn ya Sweden Kushirikiana

Posted on: July 26th, 2018

Meya wa Manispaa ya Alvsbyn (katikati) Bi Helena Ohlund na Mhe.Diwani  Severine Lasway wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo (Kulia) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano huo kushoto ni Mh.Diwani Simon Kinabo wa Rombo

Halmashauri ya wilaya ya Rombo na Manispaa ya Älvsbyn ya nchini Sweden imesaini makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano katika vipengele vitano ambavyo ni ukuaji wa miji na mipango miji, mazingira,huduma za afya kwa vijana, utalii wa asili na usalama wa chakula. Ambapo vipengele vitatu vya mazingira,usalama wa chakula na huduma za afya kwa vijana vitaanza kufanyiwa utekelezaji kuanzia mwezi wa tisa 2018.

Ushirikiano huu mpya ulioanzishwa kati ya Älvsbyn na Rombo unafadhiliwa na ICLD, Kituo cha Kimataifa cha Demokrasia ya Mitaa. Mpango huu ni kuwezesha ushirikiano kwa angalau miaka mitano, anaelezea Linda Öhlin, meneja wa mradi.

Wawakilishi wanne kutoka wilaya ya Rombo walialikwa kufanya ziara fupi katika manispaa ya Alvsbyn  mwezi mei mwaka huu. Wawakilishi hao ni Mkuu wa wilaya  Bi Agness Hokororo ambaye pia alikuwa Mkuu wa msafara, Mh.Diwani Severine Lasway (Mwenyekiti, kamati ya Elimu ,Afya na Maji), Mh.Diwani Simon Kinabo (Mwenyekiti, kamati ya Uchumi, ujenzi  na mazingira) pamoja na Mathias Gungumka ambaye ni Afisa Usafi na Mazingira wa wilaya.

Katika ziara hiyo timu ya Rombo ilijifunza mambo mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira kwa kuchakatisha taka kuwa malighafi za viwandani ambapo mbali na kutunza mazingira pia ni njia ya kuongeza kipato.

Vile vile walijifunza jinsi ya kuongeza thamani bidhaa za chakula na bidhaa nyingine kwa ubora wa viwango vya juu pamoja na upatikanaji na usambazaji wa maji salama na safi kwa kutumia teknolojia ya tarakinishi (computer) ili kupunguza gharama za uendeshaji wa sekta hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo alisema kuwa ziara ya Alvsbyn ilikuwa ya kuvutia na yenye kuongeza ujuzi na inaonekana kuwa ni sehemu yenye watu wanyenyekevu na wachapakazi ndio maana hawakuweza kuona watu wengi muda wa mchana hali ambayo ni nzuri.

"Nimevutiwa na nidhamu ya waswideni ya kuchambua na kuchakata taka. Tunahitaji kuanza kufanya kazi hiyo vizuri zaidi katika wilaya yetu ya Rombo, ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuwafanya watu waweze kubadilisha mtazamo na mawazo yao juu ya usimamizi na matumizi ya taka baada ya kuzichambua na kuzichakata”. Alisema Hokororo

Wilaya ya Rombo ina mengi ya kujifunza kutoka katika Alvsbyn ambapo tunalenga kuboresha huduma za afya, hasa kwa vijana na jambo moja muhimu ni kuzuia mimba zisizotarajiwa mapema miongoni mwa vijana.Ndugu zetu wa Alvsbyn pia wanayo mengi ya kujifunza kutoka Rombo, kwa mfano, utalii wa asili na maendeleo ya uzalishaji wa chakula cha asili ili kuongeza kiwango cha kujitegemea miongoni mwa wananchi,alimalizia Hokororo

  





Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved