ROMBO YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA ELIMU SEKONDARI (MITIHANI KIDATO CHA PILI NA CHA NNE) NA WADAU WA ELIMU.
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ikiongonzwa na Mhe. Raymond Steven Mwangwala Mkuu wa Wilaya ya Rombo (Mgeni rasmi) mapema leo imefanya kikao cha tathmini ya Elimu ya sekondari (taaluma na michezo) na wadau mbalimbali wa Elimu katika ukumbi wa shule ya msingi St. Joseph ya Mkuu.
Akizungumza Katika kikao hicho Mhe. Raymond Mwangwala aliwataka wadau wote katika kikao hicho kuhalikisha wanasimamia mustakabali wa elimu kwani elimu ndio msingi katika kujenga taifa imara.
"Tunapojadili haya tujifananishe katika ushindani wa dunia, Je elimu tunayoitoa inaendana na ushindani wa dunia? na ili kulifahamua hilo ni wazi tunahitaji kufanya vikao kama hivyi vya tathmini pamoja wadau wa Elimu lakini pia kufanya tafiti za kina zaidi ili kuboresha zaidi sekta hii ya Elimu" alizungumza Mhe. Mwangwala.
Kadhalika Mkuu wa Wilaya ameomba wadau wa elimu kona haja ya kuongeza somo la maadili kwa wanafunzi ili kukabiliana na changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa katika kipindi hiki Cha utandawazi.
Pia Mhe.Mwangwala amepongeza jitihada za wadau wa elimu katika kutambua umuhimu wa kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
"Licha ya kutambua jitihada hizo bado nawaomba waalimu wakuu kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti wake nyumbani na shuleni na kutunza miti hiyo na nitahakikisha nafanya ziara za kushtukiza kujionea hali inakwendaje" Mhe. Mwangwala amezungumza hayo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi yaliyosababishwa na uharibifu wa mazingira
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved