Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin babu amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Ndg Godwin Chacha na menejimenti ya Halmashauri kwa kuvuka lengo katika ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 118 kwa mwaka wa fedha 2023/24
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameipongeza Wilaya ya Rombo kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfulululizo.
Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali leo Julai 04, 2024 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri, Mhe Nurdin Babu amesema Wilaya ya Rombo inachangia kwa kiasi kikubwa Mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kufanya vizuri kitaifa.
Mhe Nurdin Babu amewaelekeza Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji na Waheshimiwa madiwani kuendelea kusimamia na kuhakikisha hakuzalishwi hoja zaidi ya kumi wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG Mwaka 2024/2025.
“Nataka wakuu wa idara wote washiriki kikamilifu katika suala zima la kuzuia uwepo wa hoja na kuzijibu hoja za ukaguzi, nyinyi wakuu wa idara ndio tunawategemea, muwasaidie sana waheshimiwa madiwani kuchakata na kujibu hoja zote kwa ufanisi kama mlivyofanya sasa” amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu.
“Mkurugenzi endeleeni kumuwezesha Mkaguzi wa Ndani afanye kazi yake, kwa sababu yeye ndio anajua hili tusipolitekeleza itakuwa hoja na tukitekeleza haitakuwa hoja kwa hiyo msaidieni mkaguzi wa ndani” ameongeza Mhe Nurdin Babu.
Kikao hicho cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG kimefanyika ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imewasilisha hoja tano za ukaguzi zilizojadiliwa na kutolewa maelekezo na waheshimiwa madiwani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Nurdin Babu.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved