Pichani ni Afisa Mipango(W) Bwana Chrispine Mng'anya akiwa kwenye mkutano kata za Olele,KIngachi na Kitirima kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo
Wananchi wilayani Rombo katika Kata za Olele, Kitirima na Kingachi wamekaa kwa pamoja na uongozi wao wa kata na kukubaliana kupiga vita njaa mashuleni kwa kuchangia chakula cha watoto wao ili wasome katika mazingira bora na hatimaye waweze kupata elimu bora.
Kukosekana kwa chakula mashuleni hasa katika shule za kata kunasababisha watoto kutokusoma vizuri,kushuka kitaaluma na wengine kuzurura mitaani kutafuta chakula kitu kinachopelekea wengine kujihusisha na vitendo vya udokozi.
“Jukumu la utoaji wa chakula mashuleni ni la wazazi,na hili limekuwa likifanyika kwa miaka mingi katika wilaya yetu, hivyo ni vema wazazi muendelee kuchangia,si busara sana watoto kuzagaa mtaani kutafuta chakula”, alitolea msisitizo Afisa Mipango(W) Bwana Chrispine Mng’anya katika mkutano wa kuwahamasisha wananchi kuchangia shughuli za maendeleo katika kata hizo.
Kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti baada ya tamko la Raisi kufuta michango mashuleni huku baadhi ya wazazi wakihusisha michango ya watoto wao kupata chakula shuleni kufutwa kitu ambacho si sahihi, bado ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto wake amekula shuleni ili aweze kufanya vizuri katika masomo,mtoto kusoma huku akiwa na njaa kunamsababishia kushuka kitaaluma.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved