Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Kanal Hamis Maiga aongoza kikao cha robo ya nne ya mwaka, Aprili - Juni 2023 kuhusu tathimini ya lishe leo katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya ya Rombo. Kikao hicho kilihudhuriwa na Watendaji wa kata, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Afisa tawala Afisa lishe, Afisa Sheria pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya.
Katika kikao hicho Mhe. Kanali Maiga ameagiza shule zote za msingi na sekondari ambazo bado hazitoi huduma ya chakula kuahikikisha huduma inatolewa mara moja. "Utoaji wa chakula shuleni utawapunguzia wanafunzi kukaa shuleni mda mrefu bila kula, mahudhurio kuongezeka na hata kuchangia ufaulu kwa wanafunzi" Mkuu wa Wilaya aliongeza.
Vilivile, alitoa wito kwa wazazi kuwa, pamoja na Elimu kutolewa bure, ni jukumu la wazazi kuchangia huduma ya chakula shuleni kama muongozo wa Elimu unavyoelekeza. Sambamba na hilo, aliwaagiza Maafisa Elimu Msingi na Sekondari kutoa elimu kwa wazazi hao juu ya umuhimu wa kutoa michango kwaajili ya huduma ya chakula shuleni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo akiwakilishwa na Mkuu wa Divisheni ya utawala na utumishi Ndg. Judith P Mahende, aliwataka watendaji wa kata kutekeleza maagizo mbalimbali ya lishe yanayotolewa kwa kila kata kwa wakati. Endapo watendaji hao watashindwa kutekeleza maagizo hayo, posho zao hazitalipwa hadi utekelezaji utakapokamilika.
Agizo hili lilikuja baada ya kugundulika kwa hali ya kusuasua katika utekelezaji na uwasilishaji wa taarifa kwa baadhi ya viongozi.
Imetolewa na Afisa Mawasiliano Serikalini
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved