Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh Mwl Raymond Mangwala Leo akiwa kwenye kanisa la Mtakatifu Pius x Tarakea
Amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Rombo kuwa na mshikamano na upendo na kufanya kazi kwa maendeleo ya Nchi yao.
Mangwala amesema ameshuhudia matukio ya kutisha kama kuchomana visu pamoja na kuuwana.
Amewaomba wazazi/vijana/na wazee kusaidiana nakuwa fanya watu kuwa katika maadilii mazuri na kuacha vitendo vya uhalifu.
Amewaomba ndugu jamaa na marafiki kutokukaa kimya pindi uhalifu utakapotokea kwani kuna mtu anamwona mwenzie akifanya uhalifu na kuwa kimya ivyo uleta madhara kwa wengine na kusababisha watu kutokuwa na Amani.
Amesema katika vitabu vya mungu katika Amri 10 za mungu zote zinazungumzia upendo na kuwaomba watu tupendane amesema katika vizazi vinavyokuja ni vizazi vya maaskofu mapadri masista na viongozi mashehe ivyo watu tuishi kwa upendo na kutokomeza vitendo vya uhalifu.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved