Katika ziara hiyo, Mkuu wa wilaya aliweza kukagua miradi ifuatayo :-
1. Mradi wa ujenzi wa Bweni jipya la wanafunzi la shule ya Sekondari Keni wenye thamani ya Tsh. Milioni 200 ambao upo katika hatua za mwishoni.
2. Mradi wa ujenzi wa Tenki kubwa la maji lenye ujazo wa lita laki tano za maji, wenye thamani ya Tsh. Milioni 194.8 ikiwa ni katika kuboresha huduma ya maji katika mjii mdogo wa Mkuu.
3. Mradi wa ujenzi wa Choo Shule ya sekondari Horombo katika kata ya Kelamfua Mokala ambapo mradi huu una jumla ya thamani Tsh Milion 22.4.
4. Mradi wa ujenzi wa kivuko Wama katika kata ya Ubetu Kahe. Mradi huu utakaotumia Tsh milioni 131.5 mpaka kukamilika.
5. Mradi wa Shamba Darasa la kahawa katika kata ya Ushiri Ikuini .
6. Ujenzi wa Zahanati ya Msangai katika kata ya Nanjara wenye thamani ya Tsh milioni 112.5.
7. Mradi wa kikundi cha vijana wa Tarakea Saving katika kata ya Tarakea Motamburu.
8. Mradi wa kitalu cha miti katika kata ya Motamburu Kitende.
Hata hivyo katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya akiongozana na wajumbe na viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri alisisitiza kwa miradi ambayo haijakamilika ikamilike kwa wakati ili kuendana na kasi iliyopangwa katika kuleta maendeleo.
Cc.. Imendaliwa na Afisa mawasiliano na uhusiano serikalini Wilaya ya Rombo
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved