Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Ms Magreth John ametoa agizo kwa watendaji wa kata na vijiji kutoa taatifa za mapato na matumizi kwa wananchi. agizo hilo alilitoa alipokuwa akipokea mchango wa mabati 200 kutoka kwa wafadhili waChama Cha Mapinduzi( CCM) wanaojulikana kama Rombo Development Trust ili kuezeka jengo la mradi wa zahanati ya nduweni iliyopo katika kijiji cha mbomai, mradi uliokuwa umesisimama kwa muda mrefu toka ulipoanzishwa mwaka 2014 kutokana na kusuasua kwa michango ya wananchi.
Ms Magreth aliongeza kuwa anaamini iwapo wananchi watapewa taarifa za mapato na matumizi watapata moyo zaidi wa kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo wanayoishi,
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved