Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Godwin Chacha ametoa mafunzo kwa vikundi 20 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ,kuhusu matumizi sahihi ya fedha za mikopo, uaminifu katika marejesho na njia rahisi ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo za kitaalamu.
Akizungumza katika mafunzo hayo amewaasa wanavikundi wasichukue fedha za kikundi na kupeleka nyumbani ili kufanyia matumizi binafsi au kuwapa wenza wao ,kwani kwa kufanya hivyo itasababisha kikundi kizima kupoteza uaminifu na kushindwa kufanya marejesho na matokeo yake ni Halmashauri kukipeleka kikundi mahakamani.
Sambamba na hilo Chacha ameviasa vikundi ambavyo ndio mara ya kwanza kuchukua mkopo kufuata fedha benki kwa pamoja ili kuepuka kusalitiana, iwapo ikatokea mwanakikundi mmoja au wawili wamekimbia na fedha na kupelekea kikundi kushindwa kufanya marejesho haimaanishi watasamehewa , kikundi bado kitahitajika kufanya marejesho ya mkopo.
Ameongeza kuwa serikali inatoa mikopo hiyo ambayo inatokana na 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri bila riba wala rushwa ya aina yeyote, ikiwa na lengo la kuwainua wananchi kiuchumi hivyo ni muhimu kwa vikundi kufanya marejesho kwa uaminifu ili serikali ipate nguvu ya kusaidia vikundi vingine.
Vilevile amevitaka vikundi hivyo visisite kufika ofisini na kukutana na wataalamu muda wowote wanapopata changamoto katika shughuli zao kama kikundi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu na kupata maelekezo ya kinachotakiwa kufanyika ili kutatua changamoto zao.
“Usichezee mtaji, chezea faida huku ukikumbuka kuwa faida nayo inatakiwa kuwa sehemu ya kukuza mtaji ambao utakufanya usogee kutoka katika hatua moja kwenda nyingine”, amesema Chacha
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved