• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Makamu wa Raisi Azuru Rombo

Posted on: November 10th, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wasikwepe kulipa kodi zilizoruhusiwa na serikali alipokuwa anawahutubia wananchi wa Tarakea wilayani Rombo.

“Kwa kutazama tu eneo hili ni la biashara hivyo kwa wale wafanyabiashara tulipeni kodi,kwasababu kodi zenye kuudhi wananchi serikali imeziondosha na kuzipiga marufuku, lakini zile zilizoruhusiwa mzilipe ili lipatikane fungu zuri lifanye maendeleo pote Tanzania, Serikali  hii inafanya maendeleo kwa fedha yetu wenyewe, msaada baadae”,alisema Samia

Mhe.Samia amefanya ziara  wilayani Rombo mnamo Tarehe 9.11.2018 kwa lengo la kutembelea na kukagua shughuli za maendeleo zinavyotekelezwa na serikali ya wilaya pamoja na  Halmashauri ya wilaya  na pia  kusikiliza changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Katika ziara aliyoifanya wilayani Rombo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa jengo la utawala, mradi wa maji Shimbi Mashariki pamoja na Msitu wa Rongai.

Mhe. Samia alitembelea ujenzi wa jengo la Utawala ,ambao bado haujakamilika kwasababu ya kukosekana kwa fedha, na kuahidi kuwa fedha za kumalizia ujenzi huo zitakuja  ila zinaweza kuchelewa kwa sababu changamoto ni nyingi na mahitaji ni mengi  lakini kipaumbele cha serikali ni kuboresha huduma zinazogusa wananchi moja kwa moja kama maji, elimu na afya.

Naye Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jaffo alieambatana na Mhe.Samia katika ziara hiyo alisema kuwa serikali inawajali sana wananchi ambapo ndani ya mpango wa kuboresha vituo vya Afya nchini ndani ya miezi 18 vituo 350 vya afya vimekarabatiwa na kujengwa na vinatoa huduma ya upasuaji, na kwa idadi hiyo rekodi imevunjwa kwani toka uhuru mpaka mwaka 2015 vituo vya afya 115 tu Tanzania nzima ndio vilikuwa vinatoa huduma ya upasuaji.

Aliongeza kuwa serikali imeona pia changamoto nyingine ya kutumia hospitali Teule (DDH) katika wilaya ya Rombo na katika mpango wa serkali wa kujenga Hospitali za wilaya 167, wilaya ya Rombo ni mojawapo na tayari awamu ya kwanza ya fedha hizo  shilingi 500,000,000 zimeshaingia katika akaunti ya Halmashauri.

Mhe. Samia akiwa katika mradi wa maji shimbi Mashariki alizungumza na wananchi wa vijiji vya Shimbi Mashariki na Munga ambao ni wanufaika wa mradi huo na kuwaahidi mradi utakamilika na wananchi kupata maji ifikapo mwezi wa tatu mwakani .

Aliongeza kuwa mradi ameuona na  kimebaki kitu kidogo sana cha kuunganisha maji kutoka kwenye kisima kuingiza kwenye tanki na kuweka pampu kubwa itakayopeleka kwenye tanki kubwa ili yaende kwa wananchi, hivyo kwa pamoja na Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo aliyeambatana nae katika ziara hiyo watawasiliana na Waziri wa Maji ili atafute fungu la kumalizia mradi huo.  

  “Tulipoingia madarakani tulitoa ahadi ya kuhakikisha tunapunguza au kuondosha kero ya maji nchini  na kumsogezea mama huduma ya maji  chini ya umbali wa mita 400 kwasababu tulitoa ahadi na mnajua serikali ya awamu hii inakwenda na ahadi zake  na Mhe. Rais ni mtu wa kusema na kutenda hivyo na hili atalitenda na maji yatapatikana”.amesema Samia

Mhe.Samia pia alitembelea msitu wa Rongai na kukuta mapokezi makubwa ya wananchi ambao alizungumza nao na kuwaambia lengo kubwa la kutembelea msitu huo ni kuona jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Misitu Tanzania katika kutunza mazingira na kukuza Tanzania ya viwanda.

Aidha alisema kuwa ofisi yake inayojishughulisha na mazingira Tanzania imetoa agizo kwa kila wilaya(Halmashauri ya wilaya) kuhakikisha katika eneo lake la kiutawala inapanda miti 1,500,000  kwa mwaka. Miti hiyo inaweza kuwa miti mikubwa au miti midogo ya mimea kama Kahawa ambayo mbali na kurekebisha hali ya hewa pia inapendezesha na kujenga uchumi wa nchi.

“Nimeingia Rombo nimevuta hewa nyepesi na naihisi kabisa ni hewa safi na hii inasababishwa na kutunza miti,hivyo nawasihi pandeni miti kwa wingi kwa sababu tunapoelekea Tanzania ya viwanda moshi mwingi sana huzalishwa na viwanda na ili tuweze kuishi salama, moshi huu utanyonywa na miti tutakayoipanda”, amesema Mhe. Samia



Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved