Jamii imesisitizwa kuzingatia umuhimu wa lishe bora kwa vijana wa rika balehe la miaka 10 -19 ambayo ni hatua muhimu ya ukuaji mara baada ya siku 1000 za mwanzo za maisha ya mtoto.
Rai hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Lishe Halamashauri ya Wilaya.ya.Rombo mwaka 2023, yaliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Kelamfua iliyopo Mkuu.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Deogratius Maruba, amesema kuwa suala la Lishe ni la muhimu katika afya ya binadamu lakini umuhimu unajikita zaidi kwenye hatua za makuzi ikiwemo hatua za makuzi kwa vijana wa rika balehe.
Amesema kuwa jamii inaoaswa kuzingatia lishe bora kwa vijana , kwa kuwa hatua ya ukuaji kwa vijana wa rika balehe, ndio maandalizi ya maendeleo ya mwili katika uzazi lakini maendeleo katika maandalizi ya nguvu kazi kwa maenedeleo ya kijamii na kiuchumi.
"Lishe bora kwa vijana balehe ni muhimu kwa kipindi cha miaka 10 -19 ndio fursa adhimu ya ukuaji na maendeleo ya binadamu baada ya siku elfu moja za mwanzo wa maisha ya mtoto, hatua ambayo inamuandaa kijana kuwa nguvu kazi ya Taifa." Alisema Dr. Maruba
Aidha, ameeleza kuwa vijana balehe wana umuhimu wa kuzingatia lishe kwani ndio msingi wa maendeleo ya binadamu na ya Nchi, hivyo jamii kwa ujumla wake wanapaswa kuzingatia na kichukua hatua stahiki kuhakikisha vinaja wanapata lishe bora kwa afya zao.
Naye Afisa Lishe Wilaya ameeleza dhumuni la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa katika jamii, kuhusu afya yanlishe na umuhimu wa lishe bora wa vijana hususani vijana wa rika balehe ambao ndio msingi wa nguvu kazi ya jamii na Taifa.
Ameyataja makadirio ya kidunia yanaonyesha kuna vijana Milion 1.2 wenye umri wa miaka 10-19 ambayo inaongezeka kwa kasi kubwa huku Tanzania ikikadiriwa kuwa robo ya watu wote ni vijana wa rika balehe.
Amesisitiza kuwa huduma za Afya ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo ya Nchi.
Awali maadhimisho hayo kiwilaya, yameambatana na utoaji wa huduma bure za Afya, ikiwemo upimaji wa hali ya lishe, upimaji wa Damu, ulinganisho wa Urefu na Uzito pamoja na kutoa elimu ya vyakula ya Afya na lishe yakiwa yamebeba Kauli Mbiu ya " Lishe bora kwa Vijana balehe ni chachu ya mafanikio yao"
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved