Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imeungana na Watanzania wote kusheherekea miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambapo maadhimisho hayo yamefanyika kimkoa Wilayani Rombo leo 9 Dec 2023 na kusheheneshwa na Kaulimbiu ya Mwaka isemayo Umoja na Mshikamano ni chachu ya Maendeleo ya Taifa letu.
Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Hassan Babu ambaye ndiye alikua mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amehimiza uzalendo katika Taifa letu huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda Amani ya Nchi na kuwasikiliza viongozi wao kwani kuijenga Amani ni ngumu kuliko kuibomoa.
Pia amehimiza maadili kwa watoto na vijana na kuwaasa wazazi kuwalea katika maadili yanayofaa.
Mwisho kabisa amekemea vikali ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji na kuwaasa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa letu bila kuchoka.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved