• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, DC asisitiza wajibu,Msimamizi wa Uchaguzi atoa maelekezo,Mbunge ataka ufafanuzi

Posted on: September 23rd, 2019



Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo  amesisitiza wajibu wa viongozi, watumishi na wananchi  katika uchaguzi, ili kuhakikisha unafanyika katika hali ya utengemano mkubwa,na  kutimiza lengo la serikali la kuongeza usimamizi wa mamlaka za serikali za mitaa kwa kuzingatia ubetuaji wa madaraka.

Akizungumza katika kikao maalum cha kutoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa Hokororo amewaambia wadau walioalikwa katika kikao hicho ambao ni viongozi wa taasisi na jumuiya mbalimbali, viongozi wa dini,vyama vya siasa,madiwani pamoja na watumishi wa serikali kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kanuni na miongozo iliyotolewa kuelekeza uchaguzi inatumiwa kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu.

“Mwongozo wa elimu ya mpiga kura unatuhusu sisi sote kwasababu tuna dhamana na wajibu wa kuhakikisha elimu inayotolewa ni sahihi na inazingatia mambo muhimu ambayo mwananchi anatakiwa kuelezwa bila kutoka nje ya mstari”, amesema Hokororo

Sambamba na hilo ametoa angalizo kuwa,  wananchi  wapewe  elimu na uhamasishaji  wa kwenda kujiandikisha  kupiga kura ifikapo tarehe 8 hadi 14 octoba ili watumie haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi,kwasababu baadhi yao   wanaamini  zoezi  lililofanyika Julai 2019 la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo ni kwa ajili ya uchaguzi wa dola( uchaguzi mkuu) ndilo linalotumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Naye Msimamizi  wa Uchaguzi wa jimbo la Rombo, David Rubibira alitoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019 kama kanuni  inavyoelekeza kutoa maelekezo haya kwa wadau mbalimbali wa uchaguzi , ukiwahusisha viongozi wa dini na wa vyama vya siasa.

Akitoa maelekezo hayo  Rubibira ametaja tarehe rasmi ya uchaguzi ni 24 Novemba,2019 katika vituo vyote vilivyopo katika maeneo husika, tarehe ya uandikishaji wa wapiga kura ambayo ni tarehe 8 hadi 14 octoba, nafasi za uongozi zinazogombaniwa ( uenyekiti wa kijiji, ujumbe wa halmashauri ya kijiji na uenyekiti wa kitongoji) pamoja na sifa za mgombea na mpiga kura.

Pia alitolea maelekezo ya kuchukua na kurejesha fomu  za kugombea uongozi, ukomo wa madaraka na uendeshaji wa mikutano ya kampeni za uchaguzi huku akisisitiza uchaguzi kuwa huru na haki ili kuhakikisha demokrasia inatendeka, na kukataza  vitendo vya rushwa, maneno ya kashfa na lugha za matusi, ubaguzi wa aina yeyote na kutoa maneno yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Hata hivyo Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini ambaye amehudhuria katika kikao hicho amehitaji ufafanuzi  zaidi kuhusu uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea, na  ametaka kujua ni ipi ngazi ya chini kabisa ya udhamini wa chama kwa mgombea .

Rubibira ametolea ufafanuzi zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea kwa kufuata kanuni  za uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji kanuni ya 17 kanuni ndogo ya(1) na ya  (2) zinazoeleka mgombea atachukua fomu siku ishirini na sita kabla ya uchaguzi  (29 Oktoba) na kurejesha ndani ya muda wa siku saba tangu siku ya kwanza ya uchukuaji wa fomu (29 Oktoba hadi 4 Novemba).

Aidha amefafanua kuhusu suala la udhamini wa vyama vya siasa kwa wagombea, kwa mujibu wa Mwongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambao umezingatia kwamba, kila chama kina utaratibu wake wa kuteua  au kutoa udhamini kwa wagombea wake.

l

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved