Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Tixon Nzunda (katikati) leo tarehe 27 Mei,2024 atoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Ndg. Godwin Chacha kwa usimamizi Bora wa miradi ya Maendeleo.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kufanya ukaguzi katika miradi sita ya maendeleo ambayo ni;
1.mradi wa ujenzi jengo la huduma za dharura la hospitali ya Wilaya
2. ujenzi wa bweni shule ya sekondari Maki
3. ujenzi wa bwalo na bweni shule ya sekondari Mashati
4. ujenzi wa majengo ya ofisi za tarafa ya Useri, Mashati pamoja na Mkuu.
Napenda kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo wakiwemo Madiwani na wataalam Kwa kusimamia ujenzi miradi kwani matokeo na thamani ya fedha inaonekana alisema na kuongeza Tixon Nzunda.
Kadhalika ndugu Tixon amemwelekeza Mkurugenzi kuhakikisha miradi ambayo haijakamilika ahakikishe imekamilika kwa wakati uliopangwa ili kuruhusu huduma kutolewa kwa wananchi.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved