• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Hokororo akemea rushwa kwa watumishi wa umma

Posted on: November 30th, 2018

Picha kwa hisani ya mtandao

Mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe.Agness Hokororo amekemea vitendo vya watumishi wa umma kuvutia au  kuonesha dalili za kutaka  kupewa rushwa pindi wanapotoa huduma kwa wananchi.

Akifungua semina ya siku moja ya mafunzo kwa  watumishi wa umma dhidi ya rushwa  katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo leo tarehe 30 Novemba, 2018, Hokororo amesema kuwa, mtumishi wa umma anapaswa kuwa kioo kwa kuhakikisha anakuwa msafi dhidi ya rushwa.

"Kama mtumishi wa umma ,uwe serikali kuu au serikali za mitaa, sisi ndio tunapaswa kuwa kioo kwasababu  tunajua madhara ya rushwa kwamba inachelewesha maendeleo na inapoteza haki kwa ujumla wake,wananchi wanajua rushwa ni nini na dalili zake lakini katika maeneo mengi watumishi ndio wamegeuka mwiba badala ya kioo", amesema Hokororo

Ameongeza kuwa serikali imeamua kupambana na rushwa kwa vitendo na haitaacha mkubwa wala mdogo kinachotakiwa ni wananchi wote kupata huduma kwa kufuata taratibu kwasababu kupata huduma ni haki yao ya msingi.

Naye afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Ndg Joseph Makuru  ambaye ndiye mtoa mada ameanza kwa kuwaasa watumishi kuwa wanatakiwa kubadilika badala ya kupokea rushwa  ni vema kushiriki  kuwakamata wale wanaotaka kuwapa rushwa.

Makuru ameelezea vifungu mbalimbali  vya sheria ya rushwa ya TAKUKURU ya mwaka 2007 ili kukuza ufahamu wa suala zima la rushwa kwa watumishi wa umma na kujua jinsi ya kuepukana nazo baadhi ya vifungu hivyo vinahusu kubadilisha matumizi ya fedha, rushwa katika ajira,matumizi mabaya ya mamlaka,mali zisizoelezeka upatikanaji wake na  kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia fedha.

Akitolea ufafanuzi kifungu namba 29 cha sheria ya kupambana na rushwa amesema kuwa ni kosa kisheria kubadili matumizi ya fedha za serikali na pale inapohitajika kufanya hivyo ni budi kupata kibali kutoka kwa wahusika walioleta fedha hizo ikiambatana na sababu ya msingi ya kutaka kubadili matumizi.

Kifungu namba 22, kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri; nyaraka,stakabadhi,Ankara,karatasi za kumbukumbu zinazohusu shughuli  za mwajiri zikiwa na maelezo ya uongo kwa kuandaa vikao hewa,bajeti na vifungu ambavyo havipo orodha ya majina ya washiriki na sahihi za kughushi , huu ni uhalifu mkubwa uliofanyiwa mipango ndio ukatendeka.

Hata hivyo ametolea msisitizo kuwa kuna mazingira mengi ya rushwa katika taratibu za manunuzi ya serikali, na hata kutoka nje ya kituo cha kazi bila ruhusa ya mwajiri pia ni kuhujumu uchumi na ni kosa kisheria kwa sababu serikali inalipa mshahara ikiamini mtumishi anafanya kazi kwa masaa ambayo anatakiwa kuwa kazini.

Amemalizia kwa kutoa onyo kali kwa kutumia kifungu namba 52 cha sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007 kuwa ni kosa kisheria kumtishia mtu anayetoa taarifa za rushwa TAKUKURU

 

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved