Chama cha ushirika,akiba na mikopo cha walimu wa HAI TEACHERS SACCOS wamefanya semina ya kutoa elimu kwa waajiriwa wapya wa mwaka 2024/2025 kwa kada mbalimbali katika Wilaya ya Rombo.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo lengo ni kuhamasisha watumishi kujiunga na SACCOS hiyo na kunufaika na fursa za fedha na maendeleo binafsi.Meneja wa HAI TEACHERS SACCOS Bi.Beatrice Msuya amesema umuhimu wa kujiunga na chama hicho ni kupata huduma za mikopo kwa masharti nafuu na namna bora ya kutumia mikopo kwa maendeleo binafsi.
kwa upande wake Mwenyekiti wa HAI TEACHERS SACCOS Bw.Baraka Owenya amesema chama hicho kinalenga kuwawezesha watumishi wa umma haswa walimu na kada nyingine kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.
See translation
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved