• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Bilioni 1.5 Kujenga Hospitali ya Wilaya Rombo

Posted on: October 23rd, 2018

Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Raisi wa Jamhuri  ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kutekeleza ahadi zake za kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali za wilaya kwa wilaya ambazo hazikuwa na hospitali hizo ikiwa ni pamoja na wilaya ya Rombo.

Serikali iliahidi kutoa kiasi cha fedha za kitanzania shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya na  tayari awamu ya kwanza ya fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 500 zimeshapokelewa na ujenzi utaanza mara baada ya wizara husika kujiridhisha na eneo  litakalotumika kujenga hospitali hiyo pamoja na ramani.

Taarifa ya ujio wa fedha hizo ilijadiliwa katika kikao cha kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango  cha Tarehe 23.10.2018 ambapo Mhe.Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo amewapongeza wataalamu wa Halmashauri kupitia Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa kufanya utafiti na kupata eneo litakalofaa kwa ujenzi wa hospitali katika kata ya kirongo samanga, kijiji cha Kiwanda kitongoji cha Mteri.

“Eneo hilo ni la umma na lilikua likitumika kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na serikali ya kijiji kukodisha ardhi kwa wananchi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya muda mfupi, na hilo lilikuwa likitendeka ndani ya sheria  iliyoanzisha mamlaka ya serikali za mitaa ya mwaka 1984, ambayo inatoa mamlaka ya ardhi ya kijiji kusimamiwa na serikali ya kijiji”, alisema Hokororo

Aliongeza kuwa mpango utakaofuata ni kufuata taratibu za kisheria na kuhawilisha matumizi ya ardhi hiyo, ili kuwezesha  uandaaji wa mchoro wa viwanja katika eneo hilo zoezi litakalosimamiwa na Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira hatua kwa hatua na hatimaye  umiliki wake upate Hati miliki ya muda mrefu .

Naye Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ,Evarist Silayo aliwasihi madiwani wa halmashauri kuungana  na ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na watendaji wa halmashauri na kuwa  kitu kimoja ili waweze kuzungumza na wananchi hasa katika kijiji cha kiwanda na wakulima wote waliokuwa wanakodi maeneo ya kulima katika eneo hilo kwa lengo la kuwapa taarifa ya ujenzi wa hospitali katika eneo.

Awali mpango wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo ilikuwa ni kukipandisha hadhi kituo cha afya Karume ili kuwa hospitali ya wilaya lakini serikali ilikataa ombi hilo, na badala yake  ndani ya mpango wa serikali wa kuimarisha sekta ya afya hususani afya ya Mama na Mtoto wilaya ya Rombo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 500 zilizotumika kujenga na kukarabati baadhi ya majengo katika kituo cha afya Karume na kuifanya iwe na hadhi ya hospitali.  

Hivyo, ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya Rombo utazidi kuimarisha huduma za Afya kwa wananchi wa Rombo ambao mpaka sasa wanatumia  Hospitali ya Huruma inayomilikiwa na kanisa katoliki kama hospitali teule ya wilaya ( DDH-District Designated Hospital),.







Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved