Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendesha mafunzo kwa waalimu wakuu wa shule za msingi wilayani Rombo kuhusu maboresho ya mfumo mpya wa usajili wa wanafunzi ujulikanao kama ‘PREM’ .
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wakuu wa shule za msingi kuelewa mabadiliko yaliyofanywa katika mfumo ili kuboresha mchakato wa usajili wa wanafunzi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa taarifa za elimu msingi.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na kuudhuriwa na waratibu wa elimu kata, Wakuu wa shule za msingi wilayani Rombo pamoja na viongozi wa elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.
Wataalamu kutoka NECTA wameeleza kuwa maboresho hayo yamefanyika katika mfumo mpya ujulikanao kama PREM ili kurahisisha usajili wa wanafunzi pia kutasaidia kuondoka makosa katika usajili wa wanafunzi lakini pia itarahisisha ufuatiliaji wa taarifa za wanafunzi.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved