AFISA ELIMU MKOA WA KILIMANJARO MWL:ABEL ADAM AKIZUGUMZA NA WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYA YA ROMBO
HABARI
Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Wilayani Rombo wameagizwa kuhakikisha wanasimamia vizuri taaluma ya wanafunzi,nidhamu na uzalendo.
Agizo hilo limetolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro Mwl:Abel Adam alipokuwa katika kikao cha tathimini ya ufaulu wa wanafunzi Wilaya ya Rombo kwa mwaka 2024,katika ukumbi wa shule ya msingi St.Joseph.
WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYA YA ROMBO KATIKA KIKAO CHA TATHIMI YA UFAULU KWA WANAFUNZI MWAKA 2024
Aidha Mwl:Adam amewataka wakuu hao kuhakikisha kila mwanafunzi anahudhuria masomo kikamilifu na kuwa na mazoezi katika masomo mbalimbali (Home work) na kufanya vikao vya wazazi ili kupata mrejesho wa kile kinachofanyika shuleni.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved